Thursday, December 13, 2012

Habari Kuu

Kagasheki awashukia vigogo Hifadhi Ngorongoro

Posted 15 hours ago
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki ametangaza kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) waliokwamisha mradi wa kuwasaidia wafugaji wa hifadhi hiyo ulioahidiwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2008....

Thursday, October 18, 2012


RATIBA YA MDAHALO WA KITAALUMA JUU YA SIKUKUU YA KUMUENZI BABA WA TAIFA LETU LA TANZANIA MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE
ITAKAYOFANYIKA CHUO CHA LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE, KARATU, SIKU YA JUMAPILI TAREHE 14/10/2012
MUDA
TUKIO
MHUSIKA/WAHUSIKA
01:00 – 02:00
Wageni pamoja na wajumbe wote wa mdahalo kufika mazingira ya Lioness na kuingia kwenye ukumbi wa mdahalo
wote
02:00 – 02:10
Utambulisho wa wajumbe waliohudhuria mdhahalo na ufunguzi rasmi wa mdahalo
Mwenyekiti wa mdahalo
 (Mkuu wa chuo Lioness)
02:10 – 02: 40
Mada kuwasilishwa juu ya kumbukumbu ya baba wa taifa la Tanzania. Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere
Mr Kisando Nina
( Mkuu wa Chuo Lioness)
02:40 – 03:00
Maoni kutolewa
Wajumbe upande wa meza kuu
03:00 – 03:50
Mdahalo kuendelea
wote
03:50 – 04:00
Taarifa mbalimbali, shukrani na kuhitimisha mdahalo
Viongozi/wawakilishi na mwenyekiti  kufunga mdahalo


LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE-KARATULIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE








Horizontal Scroll: MAISHA MWITU NI RASILIMALI
 





Office contacts: mobile: +2557 8616 4015                                                      11/10/2012
                                         +2557 6838 1469
                          Email: lionesswildlife@gmail.com
MWAALIKO KWENYE MDAHALO WA KITAALUMA JUU YA SIKUKUU YA KUMUENZI BABA WA TAIFA
LETU MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Husika na mada tajwa hapo juu, kwa kuzingatia umuhimu wa kuwaenzi viongozi mashuhuria na waliotumia nafasi zao katika kupigania haki, usawa na uhuru Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla, LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE KARATU imeandaa mdahalo wa kitaaluma kwa lengo la kuwakutanisha wanavyuo wa Vyuo vya kati mbalimbali hapa karatu mjini wakiwa kama wataalam chipukizi wa taifa hili kujumuika pamoja na kujadili nafasi ya baba wa taifa katika maendeleo ya taifa letu, Afrika na Duniani kwa ujumla, katika Nyanja za Kihistoria, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Mdahalo utafanyika siku ya jumapili tarehe 14/10/2012 ambayo ni siku aliyofariki dunia.
Muda wa mdahalo: 2:00 mchana hadi 4:00 jioni
Mahali: CHUO CHA LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE
“MAENDELEO YA TAIFA HUCHOCHEWA NA WANATAALUMA WAZALENDO KWA KUREJEA MITIZAMO ZA WAASISI WA TAIFA”

MKUU WA CHUO LIONESS WILDLIFE TRAINING CENTRE
Mr Kisando Nina

Friday, October 12, 2012

MAADHIMISHO YA SIKU YA MWALIMU NYERERE TAREHE 13 OKTOBA, 2012 JIJINI PRETORIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Katika kuadhimisha Siku ya Mwalimu Julius K. Nyerere, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini, kushirikiana na Jumuiya ya watanzania waishio Afrika Kusini wanafuraha kuwatangazia watanzania wote waishio Afrika Kusini kuwa kutakuwa na Maadhimisho ya Siku ya Nyerere, Baba wa Taifa, tarehe 13/10/2012 katika mpangilio wa ratiba ufuatao:-
Watanzania wote waishio Afrika Kusini, shime tujumuike pamoja.

 Imetolewa na 
 Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
 04/10/2012
You might also like:
TPBC: MIKATABA YA FRANCIS CHEKA NA PROMOTA KAIKE SIYAJI ...
ZIARA YA VIONGOZI WA CHADEMA MKOANI SINGIDA.
MADAKTARI WATANGAZA MGOMO KESHO